Mpango wa Kilimo cha Akili Waongeza ufanisi wa Uzalishaji wa Kilimo mkoani Jiangxi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 10, 2022
Mpango wa Kilimo cha Akili Waongeza ufanisi wa Uzalishaji wa Kilimo mkoani Jiangxi
Mfanyakazi akitia mbegu katika mashine ya kulima isiyoendeshwa na binadamu katika ushirika wa Kijiji cha Datian cha Wilaya ya Nanchang, Mkoa wa Jiangxi wa Mashariki mwa China, Machi 8, 2022. Wakati wa majira ya mchipuko, wasimaizi wa ushirika wa Kijiji cha Datian walianzisha miradi ya kilimo cha akili kwa kutumia mashine mbalimbali zisizoendeshwa na binadamu, hali hiyo imeinua ufanishi wa uzalishaji wa kilimo kwa kiasi kikubwa. Kwa kutumia teknolojia ya kulima kwenye mashamba makubwa, kuzalisha kwa mashine na kufanya usimamizi wa kidijitali, watu 26 tu wanaweza kuendesha mashamba ya hekta 866.7. (Xinhua/Peng Zhaozhi)
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha