Juhudi za uokoaji na misaada zaendelea katika Mkoa wa Guangxi wa China uliokumbwa na mafuriko (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 13, 2026
Juhudi za uokoaji na misaada zaendelea katika Mkoa wa Guangxi wa China uliokumbwa na mafuriko
Watu wakipita kwenye mafuriko ya maji ili kuwasilisha vitu na vifaa vya msaada wa dharura katika Kijiji cha Shishe, huko Guigang, Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, Julai 10, 2026. (Xinhua/Zhou Hua)

NANNING - Mvua kubwa iliyosababishwa na Kimbunga Maysak, kimbunga cha 10 kwa mwaka huu imezikumba sehemu mbalimbali katika Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi kusini mwa China na kusababisha maafa mfululizo.

Vikosi mbalimbali vya kukabiliana na hali ya dharura vimeunganisha juhudi zao na kufanya kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na uokoaji na utoaji msaada, kuwapangisha makazi walioathiriwa, kutoa huduma za afya ya umma, kuzuia na kudhibiti maafa, na kutoa uhakikisho wa utoaji wa vitu na vifaa.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha