Maonyesho ya Canton yafunguliwa yakiwa na idadi yenye kuvunja rekodi ya waonyeshaji bidhaa (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 16, 2025
Maonyesho ya Canton yafunguliwa yakiwa na idadi yenye kuvunja rekodi ya waonyeshaji bidhaa
Picha iliyopigwa Aprili 15, 2025 ikionyesha banda la Kundi la Kampuni za Midea la China kwenye Maonyesho ya 137 ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China mjini Guangzhou, Mkoani Guangdong, kusini mwa China. (Xinhua/Deng Hua)

Maonyesho ya 137 ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China, ambayo pia yanajulikana kwa jina la Maonyesho ya Canton, yameanza jana Jumanne mjini Guangzhou, Mkoani Guangdong, kusini mwa China, huku idadi ya waonyeshaji bidhaa za kuuzwa nje wakizidi 30,000 kwa mara ya kwanza katika historia ya maonyesho hayo maarufu duniani. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha