Meli ya utafiti wa kisayansi na utafiti wa mabaki ya kale kwenye bahari ya kina kirefu iliyoundwa kwa kujitegemea na China  yazinduliwa rasmi (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 30, 2024
Meli ya utafiti wa kisayansi na utafiti wa mabaki ya kale kwenye bahari ya kina kirefu iliyoundwa kwa kujitegemea na China  yazinduliwa rasmi
Picha hii iliyopigwa Desemba 29, 2024 ikionyesha Meli ya Tan Suo San Hao (au Meli ya Utafiti No. 3) yenye matumizi mbalimbali ya utafiti wa kisayansi na utafiki wa mabaki ya kale kwenye bahari ya kina kirefu jana Jumapili ilifika bandari moja ya Mji wa Sayansi na Teknolojia wa Ghuba ya Yazhou huko Sanya, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, na kuzinduliwa rasmi. (Picha na Li Duojiang/Xinhua)

Meli hiyo yenye urefu wa mita 104 iliyosanifiwa na kuundwa na China kwa kujitegemea ina uwezo wa kubeba karibu tani 10,000, uhimilivu wa kusafiri maili 15,000 za baharini na uwezo wa kubeba wafanyakazi 80. Na kwenye sehemu za mbele na nyuma za meli hiyo, vimewekwa vifaa vyenye uwezo wa kupasua barafu kwa mwelekeo wa pande mbili. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha