China yarusha kundi jipya la satelaiti za kuhisi kwa mbali kwenye anga ya juu (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 01, 2023
China yarusha kundi jipya la satelaiti za kuhisi kwa mbali kwenye anga ya juu
Roketi ya kubeba ya Long March-2D iliyobeba setilaiti tatu za kuhisi kwa mbali ikiruka kutoka kwenye Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Xichang kilichoko Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China, Agosti 31, 2023. (Picha na Zhang Yingjian/Xinhua)

XICHANG - China imerusha roketi ya kubeba ya Long March-2D siku ya Alhamisi kwa ajili ya kubeba na kuweka kundi la satelaiti tatu za kuhisi kwa mbali kwenye anga ya juu.

Satelaiti hizo tatu za familia ya Yaogan-39 zimerushwa Saa 9:36 alasiri (Kwa saa za Beijing) kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Xichang kilichoko katika Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China na kuingia kwenye obiti iliyopangwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha