China yarusha satelaiti mpya ya kusaidia kupambana na maafa (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 10, 2023
China yarusha satelaiti mpya ya kusaidia kupambana na maafa
Roketi ya Long March-2C iliyobeba satelaiti kusaidia kupambana na maafa ikirushwa kutoka kwenye Kituo cha kurushia Satelaiti cha Taiyuan kaskazini mwa China Agosti 9, 2023. Satelaiti hiyo imeingia kwenye obiti yake kama iliyopangwa. Urushaji huo ni urushaji wa 482 kwa kutumia roketi ya Long March. (Picha imepigwa na Lu Xing/Xinhua)

TAIYUAN, Agosti 9 (Xinhua)

China imerusha satelaiti mpya kwa ajili ya usimamizi wa kupambana na maafa kutoka kwenye kituo cha kurushia satelaiti cha Taiyuan katika Mkoa wa Shanxi.

Satelaiti hiyo ilirushwa alfajiri ya jana kwa roketi ya Long March-2C na kuingia kwenye njia iliyopangwa. Watumiaji wake wakuu watakuwa watu wa wizara ya Usimamizi wa mambo ya dharura na wizara ya Ikolojia na Mazingira.

Satelaiti hiyo itakuwa kwenye mtandao wa obiti, unaofanana na ule wa satelaiti zilizoko angani ulioanza kazi mwezi Oktoba mwaka jana, na kuunda mfumo wa awali wa satelaiti kwa ajili ya usimamizi wa dharura na usimamizi wa mazingira.

Mfumo wa rada ya kisasa uliomo ndani ya satelaiti hiyo unaweza kufanya kazi kwenye hali ya mawingu na mvua, hali ambayo inaondoa changamoto ya ufanisi kwenye satelaiti nyingine.

Mfumo wa kuchakata data kuhusu hali ya dharura kwenye satelaiti hiyo, unaweza kusaidia upigaji picha wa wakati halisi, pamoja na uchambuaji wa awali wa habari za maeneo yenye hatari.

Satelaiti hiyo itatoa data za kimsingi za kusaidia kazi ya kukabiliana na maafa, na pia kuchangia katika usimamizi wa raslimali za ardhi, uhifadhi wa maji, kilimo na misitu. Urushaji huo wa satelaiti umekuwa wa 482 kwa kutumia safu ya roketi ya Long March.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha