

Lugha Nyingine
China yarusha satelaiti mpya ya kusaidia kupambana na maafa (2)
TAIYUAN, Agosti 9 (Xinhua)
China imerusha satelaiti mpya kwa ajili ya usimamizi wa kupambana na maafa kutoka kwenye kituo cha kurushia satelaiti cha Taiyuan katika Mkoa wa Shanxi.
Satelaiti hiyo ilirushwa alfajiri ya jana kwa roketi ya Long March-2C na kuingia kwenye njia iliyopangwa. Watumiaji wake wakuu watakuwa watu wa wizara ya Usimamizi wa mambo ya dharura na wizara ya Ikolojia na Mazingira.
Satelaiti hiyo itakuwa kwenye mtandao wa obiti, unaofanana na ule wa satelaiti zilizoko angani ulioanza kazi mwezi Oktoba mwaka jana, na kuunda mfumo wa awali wa satelaiti kwa ajili ya usimamizi wa dharura na usimamizi wa mazingira.
Mfumo wa rada ya kisasa uliomo ndani ya satelaiti hiyo unaweza kufanya kazi kwenye hali ya mawingu na mvua, hali ambayo inaondoa changamoto ya ufanisi kwenye satelaiti nyingine.
Mfumo wa kuchakata data kuhusu hali ya dharura kwenye satelaiti hiyo, unaweza kusaidia upigaji picha wa wakati halisi, pamoja na uchambuaji wa awali wa habari za maeneo yenye hatari.
Satelaiti hiyo itatoa data za kimsingi za kusaidia kazi ya kukabiliana na maafa, na pia kuchangia katika usimamizi wa raslimali za ardhi, uhifadhi wa maji, kilimo na misitu. Urushaji huo wa satelaiti umekuwa wa 482 kwa kutumia safu ya roketi ya Long March.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma