Wanaanga wa China kwenye Chombo cha Shenzhou-15 wamaliza matembezi ya nne kwenye anga ya juu, na kuweka rekodi ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 17, 2023

https://english.news.cn/20230416/350767d9534446b09b1e7bc812506270/aa5b878960d840788f5e6d44c27aa71c.jpg

Picha hii iliyopigwa kwenye skrini katika Kituo cha Udhibiti wa Anga cha Beijing Aprili 15, 2023 ikionyesha mwanaanga wa China kwenye Chombo cha Shenzhou-15 Zhang Lu akipunga mkono baada ya kufanya shughuli nje ya moduli ya maabara ya Wentian. (Xinhua/Guo Zhongzheng)

BEIJING - Wanaanga wa China kwenye Chombo cha Shenzhou-15 kwenye kituo cha anga ya juu cha Tiangong cha China kinachozunguka wamekamilisha matembezi yao ya nne kwenye anga ya juu, Shirika la Anga ya Juu la China limesema Jumapili.

Fei Junlong na Zhang Lu, pamoja na Deng Qingming ambaye alifanya kazi ndani ya kituo hicho cha anga ya juu na timu ya usaidizi ya duniani, walishirikiana kumaliza kazi zote zilizopangwa Jumamosi. Fei na Zhang wamerejea salama kwenye moduli ya maabara ya Wentian.

Mpaka sasa Wanaanga hao watatu wamefanya shughuli nje ya kituo cha anga ya juu kwa mara nne tangu walipotumwa kwenye anga ya juu Novemba 2022, na kuweka rekodi ya China ya matembezi mengi zaidi kwenye anga ya juu kwa mwanaanga mmoja wa kikundi cha wanaanga.

Wakati wa shughuli hizo za hivi karibuni, walifunga vifaa kadhaa, ikiwa ni pamoja na seti za pampu zilizopanuliwa za ziada, kebo za kuvuka moduli, na vifaa vya kusaidia kwenye jukwaa la upakiaji wa vifaa vya shughuli nje ya kituo cha anga ya juu cha China, wakiweka msingi wa kufanya majaribio makubwa ya baadaye ya sayansi na teknolojia nje ya kituo cha anga ya juu, shirika hilo limeeleza katika taarifa yake. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha