Chombo cha kwanza cha “Fuyao” cha mashine za kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo kwenye bahari kuu chazinduliwa Guangdong, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 30, 2022
Chombo cha kwanza cha “Fuyao” cha mashine za kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo kwenye bahari kuu chazinduliwa Guangdong, China
Picha iliyopigwa kutoka angani Mei 29, 2022 ikionesha chombo cha “Fuyao” cha mashine za kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo kikielea kwenye bahari ya kina kirefu kimevutwa kutoka Maoming hadi eneo la bahari la Luodousha, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. Chombo hicho cha kwanza kiitwacho "Fuyao" cha mashine za kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya upepo kinachoelea kwenye Bahari ya China kimevutwa huko Maoming, Mkoa wa Guangdong Kusini mwa China jana Jumapili, kitafanyiwa majaribio ya kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo katika eneo la bahari la Luodousha ambalo lina wastani wa kina cha maji cha mita 65. Chombo hicho kimefungwa mashine za kustahimili kimbunga zenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 6.2. (Xinhua/Liu Dawei)
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha