

Lugha Nyingine
Kituo cha Uzalishaji wa Umeme kwa mwanga wa jua cha Yunnan, China chatoa nafasi za Ajira na kuongeza Kipato cha Wanavijiji
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 18, 2022
Picha iliyopigwa kutoka angani Februari 16 ikionesha kituo cha uzalishaji wa umeme kwa mwanga wa jua cha Wilaya ya Yongren ya Mkoa wa Yunnan ulioko Kusini Magharibi mwa China. Wilaya hiyo ikitumia maliasili yake ya kutosha ya nishati ya jua, imezialika kampuni kuja huko kujenga vituo vya uzalishaji wa umeme kwa kutumia mwanga wa jua, hivyo kutoa ajira na kuongeza kipato kwa wanavijiji huko. Mpaka hivi sasa, vituo vya uzalishaji wa umeme kwa mwanga jua zaidi ya 112 vimejengwa katika wilaya hiyo, na thamani ya jumla ya uzalishaji wa umeme imefikia Yuan za Renminbi bilioni 1.6 (takribani Dola za Marekani milioni 252.64). (Xinhua/Chen Xinbo)
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma