Bandari za China zashuhudia ukuaji katika biashara na nje (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 24, 2026
Bandari za China zashuhudia ukuaji katika biashara na nje
Picha iliyopigwa Novemba 19, 2026, ikionesha meli ya mizigo ikiwa imetia nanga kwenye gati la makontena la Eneo la Bandari la Chuanshan la Bandari ya Zhoushan ya Ningbo katika Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China. (Xinhua/Huang Zongzhi)

Takwimu zilizotolewa na Idara ya Takwimu ya Kitaifa ya China zimeonesha kuwa, katika miezi kumi ya kwanza ya mwaka 2026, thamani ya bidhaa zilizoagizwa na kuuzwa nje ya China ilifikia yuan trilioni 44.81 kwa jumla (dola za Marekani takriban trilioni 6.68), ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 20 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa, tokea mwanzo mwa mwaka huu, kiasi cha jumla cha bidhaa zilizoagizwa na kuuzwa nje cha China kimedumisha ukuaji wa kasi, muundo wa biashara umeendelea kuboreshwa, na njia za usafirishaji wa kimataifa zinaendelea kuwa na hali isiyo na utata zaidi; hali ambayo imeonesha uhimilivu na nguvu hai za uchumi wa China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha