Mazungumzo kati ya watu wa China na Afrika ya 2026 yafanyika Mauritius

(CRI Online) Novemba 23, 2026
Mazungumzo kati ya watu wa China na Afrika ya 2026 yafanyika Mauritius
(Picha/Xinhua)

Mazungumzo kati ya watu wa China na Afrika ya 2026 yalifanyika kuanzia Novemba 18 hadi 20 huko Port Louis, mji mkuu wa Mauritius, yakihimiza zaidi mawasiliano kati ya watu wa China na Afrika kutoka nyanja zote za maisha.

Mazungumzo hayo yaliyoandaliwa kwa pamoja na Shirika Lisilo la Kiserikali la China Mtandao wa Mawasiliano ya Kimataifa na Baraza la Uchumi, Jamii na Utamaduni la Umoja wa Afrika, chini ya kaulimbiu “Kutoka Mazungumzo hadi Hatua za Utekelezaji: Ushirikiano Unaoongozwa na Raia kwa Mustakabali wa Pamoja," yamewaleta pamoja washiriki zaidi ya 200 kufanya majadiliano ya kina juu ya kuimarisha mawasiliano kati ya watu, kujenga majukwaa ya ushirikiano, na kuhimiza uhusiano wa karibu kati ya watu wa China na Afrika.

Washiriki hao wanaona kuwa mawasiliano kati ya watu ni msingi wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika. Pande mbili zinapaswa kushikilia kutanguliza maslahi ya watu, kuendelea kuchunguza mawasiliano na ushirikiano kwenye nyanja nyingi muhimu, na kutafsiri makubaliano yaliyofikiwa na pande mbili kuwa matokeo halisi yanayoleta manufaa kwa watu wa pande mbili, na kukuza urafiki kati ya watu wa pande mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha