Meli kubwa ya Pili ya Utalii ya China Yaanza Usafiri Wake wa Kwanza wa Kibiashara (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 23, 2026
Meli kubwa ya Pili ya Utalii ya China Yaanza Usafiri Wake wa Kwanza wa Kibiashara
Watu wakiitazama Adora Flora City, meli kubwa ya pili ya abiria iliyoundwa nchini China wakiwa kwenye jukwaa la kutazamia la Bandari ya Kimataifa ya Meli za Abiria ya Nansha ya Guangzhou . (Picha na Xu Jianmei/Xinhua)

GUANGZHOU - Meli kubwa ya pili ya utalii iliyoundwa nchini China Adora Flora City, imeanza usafiri wake wa kwanza jana Jumapili, ikionesha hatua mpya katika juhudi za China za kupanua shughuli za utalii za meli na kuchochea matumizi.

Meli hii inayobeba abiria zaidi ya 3,800, imeondoka Guangzhou katika Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, na itasafiri kwa siku sita na usiku tano kuelekea Hong Kong na Hue, Vietnam.

Meli hiyo yenye urefu wa mita 341 na uzito wa tani 141,900, kwa jumla ina vyumba 2,130 vya abiria na uwezo wa kubeba abiria wapatao 5,232 hivi.

Uundaji wa Adora Flora City ulianza mwezi Agosti 2022. Meli hiyo, inayoendeshwa na kampuni ya Adora Cruises chini ya Kundi la Utalii la China, tarehe 6 mwezi huu ilikabidhiwa mjini Shanghai, mashariki mwa China, na ilifanya usafiri wake wa kwanza wa majaribio tarehe 9 Novemba.

Shi Dai, meneja mkuu wa Kundi la Utalii la China, amesema kampuni hiyo inatumia shughuli za uendeshaji wa meli za utalii kuhimiza maendeleo ya shughuli za jumla za utalii wa kiutamaduni na uzoefu wa kusafiri, ikilenga kuweka kiwango kipya kwa likizo baharini.

Adora Flora City ni meli kubwa zaidi, na usanifu wake ulipangiliwa kwa ustadi zaidi kuliko meli pacha yake, Adora Magic City, ambayo ni meli kubwa ya kwanza ya kitalii iliyoundwa nchini China. Adora Magic City ilianzisha shughuli zake za usafiri wa kibiashara Januari 2024, na tokea wakati huo mpaka sasa imekamilisha usafiri wake kwa mara 250 hivi.

Hu Zhenyu, Naibu Mkurugenzi wa tawi la Qianhai la Taasisi ya Maendeleo ya China, amesema kuanza kutumika kwa meli hizo mbili kubwa za kitalii zilizoundwa nchini China kumeonesha kuwa maendeleo ya shughuli za meli za utalii nchini China yameingia katika kipindi kipya.

Hu amesema, "Maendeleo haya si tu yataongeza shughuli mbalimbali za utalii kwenye bahari zenye sifa bora ya juu, bali pia yataleta msukumo mpya kwa matumizi katika maeneo ya pwani."

Mwaka 2027, meli ya hiyo ya Adora Flora City imepangwa kufanya usafiri kwa mara zaidi ya 50 kwenda nchi mbalimbali duniani kutoka bandari yake ya nyumbani mjini Guangzhou, na usafiri wake utakuwa wa muda mfupi wa wikend na safari ndefu kuelekea nchi za Vietnam, Malaysia, na Brunei.

Meli hiyo pia itafanya usafiri bila kupangiwa kusimama kwenye bandari nyingine, ili kuwawezesha abiria kufurahia kukaa kwenye meli hiyo yenyewe kama mahali pa kutalii.

Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Maliasili ya China zimeonesha kuwa, shughuli za utalii za kupanda meli za abiria zimepata ongezeko zaidi, na idadi ya jumla ya abiria wa meli hizo ikiongezeka kwa asilimia 25.3 mwaka 2025 ikilinganishwa na mwaka 2024.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha