Lugha Nyingine
Tamasha la Teknolojia la Afrika lafunguliwa Cape Town likizingatia fursa za AI (2)
Tamasha la Teknolojia la Afrika la mwaka 2026 limefunguliwa huko Cape Town, Afrika Kusini, likilenga kuhimiza mabadiliko ya kidijitali barani Afrika na kuiwezesha Afrika kutumia fursa katika zama ya AI.
Tamasha hilo ni moja kati ya shughuli kubwa zaidi za kiteknolojia barani humo, likiwaleta pamoja viongozi kutoka sekta za mawasiliano ya simu na teknolojia, wajasiriamali, wawekezaji, watunga sera na wabunifu kutafuta teknolojia zinazoibuka, kukuza ushirikiano, na kuhimiza maendeleo ya kidijitali barani humo.
Tamasha la mwaka huu lenye kaulimbiu ya “Kuhimiza Mabadiliko ya Kidijitali ya Afrika” litaendelea hadi Alhamisi, likiwa na washiriki zaidi ya 13,500 na kampuni 2,000 kutoka nchi zaidi ya 130, watoa hotuba 450, na waoneshaji 350.
Shughuli hiyo ina nguzo sita zikiwemo mawasiliano ya simu na muunganiko, vituo vya data, AI, usalama mtandaoni, makampuni chipukizi na mabadiliko ya kidijitali, ikihusisha maeneo makuu kuanzia miundombinu ya kidijitali, teknolojia zinazoibuka hadi ujasiriamali na ukuaji wa uchumi wa kidijitali wa Afrika.

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China

Shughuli ya Siku ya Meli ya "Xuelong 2" ya China kufunguliwa kwa umma yafanyika Hainan
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
