Lugha Nyingine
Bandari ya Qingdao yapanua mtandao wa usafirishaji kwa meli na wanachama wa APEC
![]() |
| Picha hii iliyopigwa tarehe 17 Novemba 2026 ikionesha gati la makontena katika Bandari ya Qingdao, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China. (Xinhua/Li Ziheng) |
Bandari ya Qingdao katika Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China imekuwa ikiongeza kwa mfululizo idadi ya njia kwenye mtandao wake wa njia za usafirishaji kwa meli ambao unaunganisha wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC), jambo ambalo limejidhihirisha katika ongezeko kubwa zaidi la mzigo wa kuagizwa na kuuzwa nje hadi sasa mwaka huu.
Hadi sasa, Bandari hiyo ya Qingdao inaendesha njia takriban 240 za biashara ya nje, ambapo kati yake asilimia karibu 60 zinahusisha wanachama wa APEC ili kuwezesha biashara rahisi na yenye ufanisi zaidi kati ya China na washirika wake wa APEC.

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China

Shughuli ya Siku ya Meli ya "Xuelong 2" ya China kufunguliwa kwa umma yafanyika Hainan
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
