Chombo cha kubeba wanaanga cha China cha Shenzhou-24 na roketi vyapelekwa eneo la kurushia (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 18, 2026
Chombo cha kubeba wanaanga cha China cha Shenzhou-24 na roketi vyapelekwa eneo la kurushia
Picha hii iliyopigwa Novemba 17, 2026 ikionesha muunganiko wa chombo cha kubeba wanaanga kwenda anga ya juu cha Shenzhou-17 na roketi ya kubeba ya Long March-2F kwa pamoja vikihamishiwa hadi eneo la kurushia. (Picha na Fang Gaosen/Xinhua)

JIUQUAN - Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA) limesema, muunganiko wa chombo cha kubeba wanaanga cha China cha kwenda anga ya juu cha Shenzhou-24 na roketi ya kubeba ya Long March-2F kwa pamoja vimehamishiwa hadi eneo la kurushia jana Jumanne, na chombo hicho kimepangwa kurushwa kwa wakati unaofaa.

CMSA imeeleza kuwa vifaa na miundombinu yote katika eneo la kurushia viko katika hali nzuri na kwamba ukaguzi mbalimbali wa ufanyaji kazi na majaribio ya pamoja kabla ya kurushwa chombo hicho vitafanyika kama ilivyopangwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha