Lugha Nyingine
Wafanyabiashara na wanasiasa zaidi ya 2,000 wakusanyika Shenzhen kwa Mkutano wa Watendaji Wakuu wa APEC 2026 (2)
SHENZHEN – Wawakilishi zaidi ya 2,000 wa biashara na siasa wamekusanyika Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, China, jana Jumanne kuhudhuria Mkutano wa Watendaji Wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC) 2026.
Wanatoka katika nchi na chumi wanachama 21 wa APEC na 13 zisizo wanachama wa APEC, zikiwemo Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Uswisi.
Mkutano huo ambao ni sehemu muhimu ya Wiki ya Viongozi wa Uchumi wa APEC 2026, umefanyika chini ya kaulimbiu ya "Kustawi na Kushinda Mustakabali wa Siku za Baadaye Pamoja", na umefanyika Novemba 17 na 18 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Qianhai.
Kwenye hotuba yake ya ukaribisho, Ren Hongbin, mwenyekiti wa Baraza la China la Kukuza Biashara ya Kimataifa na mwenyekiti wa Mkutano wa Watendaji Wakuu wa APEC 2026, ameelezea matumaini yake kwamba mazungumzo hayo yatachochea mawazo mapya na kujenga maafikiano mapana, na kuingiza msukumo mpya katika jumuiya ya Asia-Pasifiki na ukuaji duniani.
Wahudhuriaji wamejadili mazingira mapya ya uchumi wa Asia na Pasifiki na fursa za ushirikiano, huku ajenda ya mkutano ikijumuisha mada ndogo saba: kuandaa mpango mpya wa muunganisho, kujenga mfumo wa kiikolojia wa uvumbuzi wa AI ulio wazi na wenye manufaa kwa wote, kuweka mfumo mpya kwa ajili ya maendeleo endelevu katika Asia na Pasifiki, kuendeleza kwa pamoja Eneo la Biashara Huria la Asia na Pasifiki, kuchunguza njia mpya za ushirikiano wa uchumi wa kidijitali, Eneo Kuu la Ghuba ya Guangdong-Hong Kong-Macao na fursa za maendeleo ya Asia na Pasifiki, na kusukuma mbele mabadiliko ya kidijitali na kijani kwa uratibu.

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China

Shughuli ya Siku ya Meli ya "Xuelong 2" ya China kufunguliwa kwa umma yafanyika Hainan
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
