Lugha Nyingine
Walimu kutoka Karakana ya Luban nchini Ethiopia wapata mafunzo mjini Tianjin, China (6)
Mafunzo ya mradi wa uvumbuzi wa uhandisi kwa walimu kutoka Karakana ya Luban nchini Ethiopia yamefanyika hivi karibuni katika Chuo Kikuu cha Teknolojia na Elimu mjini Tianjin, kaskazini mwa China.
Mafunzo hayo yaliyolenga kufungamanisha kwa karibu uzoefu wa China wa maendeleo ya elimu ya ufundi stadi na maendeleo ya Ethiopia, kuongeza kwa pande zote ujuzi wa ufundi na uwezo wa kutoa mafunzo wa washiriki. Yamehusisha mihadhara maalum, mazoezi ya ujuzi katika vitendo, na ufundishaji wa moja kwa moja katika mazingira halisi ya kazi.
Karakana ya Luban nchini Ethiopia ilianzishwa mwaka 2021 kwa ushirikiano na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi na Kazi cha Ethiopia (TVTI), ikijikita katika maeneo muhimu kama vile vihisi vya viwandani, mekatroniki, na roboti za viwandani, wakati huohuo inaandaa kundi kubwa la wataalamu wenye ujuzi wa ufundi kwa ajili ya maendeleo ya viwanda ya Ethiopia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




