Mji wa Baoshan, China wahimiza mabadiliko ya muundo na uboreshaji wa sekta ya kahawa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 12, 2026
Mji wa Baoshan, China wahimiza mabadiliko ya muundo na uboreshaji wa sekta ya kahawa
Picha iliyopigwa Novemba 11, 2026, ikionesha kituo cha shamba la kilimo cha kahawa huko Lujiangba katika Eneo la Longyang la Mji wa Baoshan, Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China. (Xinhua/Jiang Wenyao)

Mji wa Baoshan katika Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China ambao ni eneo muhimu la uzalishaji wa kahawa yenye ubora wa juu ya punje ndogo, hivi karibuni umekuwa ukichukua hatua za kuhimiza mabadiliko ya muundo na uboreshaji wa sekta ya kahawa kutoka kuwa kituo cha malighafi hadi kuwa kituo cha maendeleo ya sekta ya kahawa yenye ubora wa hali ya juu, yenye chapa na ya utandawazi.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa, katika robo tatu za kwanza za mwaka huu, eneo la kilimo cha kahawa ya punje ndogo katika mji huo wa Baoshan lilifikia ukubwa wa hekta 12,600 hivi, likiwa na uzalishaji wa kahawa wa tani 26,400 na thamani ya jumla ya uzalishaji imefikia yuan bilioni 15.7 (dola takriban bilioni 2.35 za Marekani).

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha