Uchaguzi wa serikali za mitaa wafanyika nchini Afrika Kusini (8)

(CRI Online) Novemba 05, 2026
Uchaguzi wa serikali za mitaa wafanyika nchini Afrika Kusini
(Picha/Xinhua)

Uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Afrika Kusini umeanza jana Jumatano kwa vituo vya kupigia kura kufunguliwa saa moja asubuhi kwa saa za huko, huku zaidi ya watu milioni 29 waliojiandikisha kupiga kura wakitarajiwa kupiga kura zao katika vituo 23,700 kote nchini humo.

Vituo vya kupigia kura vilipangwa kufungwa saa tatu usiku kwa saa za huko, na matokeo rasmi kutangazwa baada ya Tume Huru ya Uchaguzi (IEC) kukamilisha mchakato wa kuhesabu na kuhakikisha kura.

Tume hiyo imesema, uchaguzi wa mwaka huu ni wa sita kwa serikali za mitaa nchini Afrika Kusini tangu nchi hiyo ilipoingia kwenye mfumo wa demokrasia mwaka 1994.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha