Walinda amani 464 wa China nchini Lebanon wapokea kwa fahari Nishani ya Amani ya Umoja wa Mataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 05, 2026
Walinda amani 464 wa China nchini Lebanon wapokea kwa fahari Nishani ya Amani ya Umoja wa Mataifa
Tarehe 3 Novemba 2026, kambi ya kikosi cha kulinda amani cha China katika kijiji cha Hanniyah, kusini mwa Lebanon, ilifanya gwaride la kutunukia nishani. (Xinhua/Ali Hashisho)

Jumla ya askari polisi 464 wa kikosi cha 24 cha kulinda amani cha China kilichotumwa Lebanon walitunukiwa Nishani ya Amani ya Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne wiki hii, kwa kujitolea kwao kulinda utulivu na amani katika eneo la kusini mwa nchi hiyo.

Hafla ya kutunukia nishani ilifanyika katika kambi ya kikosi cha kulinda amani cha China katika kijiji cha Hanniyah, kusini mwa Lebanon, ili kuwapongeza kikosi hicho chini ya Jeshi la Muda la Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL).

Katika hotuba yake kwenye hafla hiyo, Mkuu wa ujumbe maalumu na kamada wa jeshi la UNIFIL, Diodato Abagnara, alisifu mwitikio wa haraka, hatua na vitendo vya kufuata hali halisi na utendaji operesheni wa kasi wa walinda amani wa China, akiwaita "wanaotatua matatizo" na wenye nguvu muhimu ya kuweza kuhimiza utekelezaji jukumu kupata mafanikio makubwa katika wakati muhimu.

Kikosi cha 24 cha kulinda amani cha China kilianza kutekeleza jukumu la ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuanzia Desemba 2025, na kikosi hicho kinahusisha vitengo vya uhandisi, ujenzi na matibabu.

Mpaka hivi sasa, walinda amani wa China wameondoa mabomu chini ya ardhi kwenye maeneo yenye ukubwa wa zaidi ya mita za mraba 825, ambapo mabomu 146 yaliyowekwa chini ya ardhi yaliondolewa nao kwa usalama, na pia wametoa huduma za matibabu kwa walinda amani wa jeshi la UNIFIL na wakazi wa eneo hilo zaidi ya 3,400 kwa jumla.

Tokea mwaka 2006, China imetuma zaidi ya walinda amani 8,800 nchini Lebanon.

Jeshi la UNIFIL lilianzishwa mwaka 1978 kwa lengo la kuhakikisha Israel inaondoa jeshi lake kutoka Lebanon. Baada ya vita kati ya Hezbollah na Israel mwaka 2006, azimio la 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipanua jukumu la jeshi la UNIFIL ili kufuatilia kusimamishwa kwa mapigano na kufuatana na vikosi vya Lebanon vinavyopelekwa kusini mwa Lebanon wakati Israel inapoondoa jeshi lake.

Mnamo Agosti 2025, Baraza la Usalama liliongeza kwa mara ya mwisho muda wa jukumu la jeshi la UNIFIL hadi tarehe 31 Desemba 2026, na baada ya hapo jeshi hilo litakamilisha kazi yake ya kupunguza askari wake na kuondoka Lebanon ndani ya mwaka mmoja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha