Lugha Nyingine
Mji wa Changzhou, China wajenga kundi la viwanda vya pikipiki janja za kutumia umeme lenye mnyororo kamili wa utoaji bidhaa (7)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 29, 2026
![]() |
| Mhandisi akirekebisha hitilafu kwenye pikipiki ndani ya kampuni ya pikipiki janja za kutumia umeme ya Changzhou mkoani Jiangsu, mashariki mwa China, Oktoba 14, 2026. (Xinhua/Li Bo) |
Katika miaka ya hivi karibuni, Mji wa Changzhou ukitumia nguvu yake bora ya utengenezaji bidhaa umeharakisha ujengaji kundi la viwanda vya kuzalisha pikipiki janja za kutumia umeme, na wanaozalisha vipuri vyao, ukilenga maendeleo ya bidhaa bora na za hali ya juu.
Mji huo kwa sasa unachukua asilimia 10 hivi ya uzalishaji wa pikipiki zote za kutumia umeme nchini China na umeanzisha mnyororo kamili wa viwanda kutoka kazi ya vipuri hadi uunganishaji na ukamilishaji wa pikipiki.
Mji wa Changzhou pia umefanya juhudi za kuufanya uvumbuzi wa teknolojia kuwa msukumo mkuu wa maendeleo ya viwanda, na viwanda vya uundaji wa pikipiki wa mji huo vikiendelea kuongeza juhudi za kufanya utafiti na maendeleo (R&D) ili kuboresha zaidi bidhaa zao.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




