Lugha Nyingine
Kuona Siku za Baadaye Shenzhen, China | Mustakabali wa Kaboni-Sifuri Wawa Dhahiri (6)
![]() |
| Kifaa cha kupikia cha kutumia umeme na cha kaboni-sifuri kilichotengenezwa na kampuni ya China kikioneshwa kwenye Kituo cha Huduma za Kimataifa kwa Kampuni Ndogo na za Kati kilichopo eneo la Longgang, Shenzhen. (Picha na Zhou Jielu/People’s Daily Online) |
SHENZHEN — Kwa kuunganisha mazingira ya kiikolojia ya milima, bahari, na mji—pamoja na teknolojia ya kutoa kaboni chache, mji wa Shenzhen wa China unabadilisha dhana ya "kaboni-sifuri" kuwa uhalisia dhahiri na wa kila siku.
Misitu ya mikoko katikati ya mji inafanya kazi ya kuwa vifyonzaji asilia vya kaboni; viwanda vya kuzalisha nishati kutokana na taka vimebadilishwa na kuwa "bustani za nishati" zilizojificha ndani ya vilima vya kijani; usanifu wa majengo unaozingatia mazingira unaruhusu mandhari ya mji kuendana na mazingira ya asili; na kampuni zinazopanuka kwenye masoko ya kimataifa zimeifanya dhana ya "kaboni-sifuri" kuwa faida kuu ya uwezo wa kushindana kwa bidhaa zao.
Hivi karibuni, ujumbe wa waandishi wa habari kutoka China na mataifa mengine, walioshiriki katika ziara ya utafiti na mahojiano iliyopewa jina la "Kuikaribisha APEC: Kuitazama Shenzhen," walitembelea mji huo ili kujionea—kupitia lenzi zao—picha halisi za upigaji hatua wa Shenzhen kuelekea mustakabali wa "kaboni-sifuri" katika nyanja mbalimbali za ikolojia, viwanda, na maisha ya kila siku.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




