Kundi la kwanza la vitu vya kuoneshwa kwenye Maonesho ya 9 ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) lawasili Shanghai (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 27, 2026
Kundi la kwanza la vitu vya kuoneshwa kwenye Maonesho ya 9 ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) lawasili Shanghai
Hafla ya kuadhimisha kuwasili kwa kundi la kwanza la vitu vya kuoneshwa kwenye Maonesho ya 9 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) ikifanyika kwenye Kituo cha Kitaifa cha Maonesho na Mikutano (Shanghai), ukumbi mkuu wa maonyesho hayo, mjini Shanghai, mashariki mwa China, tarehe 26 Oktoba 2026. (Xinhua/Fang Zhe)

Kundi la kwanza la vitu vya kuoneshwa kwenye Maonesho ya 9 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) limewasili mjini Shanghai, mashariki mwa China. Kundi hilo linajumuisha vifaa vya kiteknolojia, vifaa tiba, na bidhaa za kilimo na chakula; ambavyo baadhi yake vitaoneshwa kwa mara ya kwanza kwenye maonesho hayo.

Kwa sasa maandalizi ya Maonesho hayo ya 9 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yanaendelea kwa bidii zote. Maonesho hayo yamepangwa kufanyika kwenye Kituo cha Kitaifa cha Maonesho na Mikutano (Shanghai) kuanzia tarehe 5 Novemba hadi 10 Novemba mjini Shanghai.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha