Baqen, Xizang: Kuweka nyaya za umeme kwenye nyumba za muda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 26, 2026
Baqen, Xizang: Kuweka nyaya za umeme kwenye nyumba za muda
Tarehe 25 Oktoba, nyaya zikichaguliwa na kupangwa na wafanyakazi wa Kampuni ya Utoaji wa Umeme ya Qamdo chini ya Kampuni ya Umeme ya Xizang ya Gridi ya China katika eneo la makazi ya muda la Kijiji cha Zharuogai, Tarafa ya Maru, Wilaya ya Baqen.

Hivi sasa, uwekaji wa nyaya za umeme katika makazi ya muda unaendelea katika eneo la Baqen lililoathiriwa na tetemeko la ardhi mkoani Xizang, China.

Kampuni ya Gridi ya China ilijulisha kuwa, imepeleka zana na vifaa vya kuunganisha umeme kwa ajili ya makazi ya muda ya mahema 2,724 na seti 2,400 za nyumba za muda, ili kukidhi mahitaji ya sasa ya uunganishaji wa umeme katika eneo la Baqen lililokumbwa na tetemeko la ardhi.

(Xinhua/Tenzin Nyida)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha