Mwendesha wa mgahawa aenda na kilo 1,500 za Jiaozi kuelelea Baqen, eneo lililokumbwa na tetemeko la ardhi (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 26, 2026
Mwendesha wa mgahawa aenda na kilo 1,500 za Jiaozi kuelelea Baqen, eneo lililokumbwa na tetemeko la ardhi
Tarehe 24 Oktoba 2026, waokoaji wakila jiaozi katika kituo cha muda cha makazi huko Tarafa ya Maru ya Wilaya ya Baqen ya mji wa Nagqu, Mkoa unaojiendesha wa Xizang. (Xinhua/Tenzin Nyida)

Alhamisi ya wiki iliyopita, baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 kwenye kipimo cha Richter kutokea katika Wilaya ya Baqen, huko Nagqu mkoani Xizang, Du Guoping, mwendesha mgahawa wa Jiaozi (chakula cha Kichina) huko Xigaze, aliahirisha siku za kuzinduliwa kwa migahawa yake miwili mipya na kwenda kwenye eneo lililoathiriwa akiwa pamoja na wafanyakazi wake.

Bw. Du alisema: "Tulichukua muda wa dakika 10 tu kuamua kwenda Baqen kuwapikia jiaozi waathiriwa wa tetemeko la ardhi."

Usiku wa manane wa siku ya tetemeko hilo la ardhi, timu ya uokoaji ilipakia zaidi ya kilo 1,500 za jiaozi kwenye magari na kuondoka Xigaze.

Baada ya kufika eneo hilo, Du na wafanyakazi wake waliweka vyombo vya kupikia na kuwaandalia jiaozi wafanyakazi wa uokoaji na wakaazi walioathiriwa na maafa.

"Ni lazima kuhakikisha kila mtu anapata jiaozi kwa kutosha, na wape watoto nyingi zaidi," Bw. Du aliwaambia wafanyakazi wake mara kwa mara.

"Tutapika jiaozi zote tulizozileta," alisema Du. " Tunaona fahari kuweza kutoa mchango wetu kwa tunavyofanya wenyewe."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha