Lugha Nyingine
Shajara ya Shenzhen, China katika siku ya tatu: Roboti, AI na Taka Kugeuzwa kuwa Umeme; Mistakabali Miwili Muhimu katika Mji Mmoja (5)
![]() |
| Mandhari ya ndani ya mtambo wa kuchakata taka ili kuzalisha umeme kwenye Bustani ya Ikolojia ya Nishati ya Longgang mjini Shenzhen, China. (People’s Daily Online) |
Jana Jumatano Oktoba 21 katika siku yangu ya tatu mjini Shenzhen, China nilihisi kama kupiga hatua kuingia kwenye mistakabali miwili muhimu sana katika mji mmoja, ikiihakikishia dunia kwamba uendelevu na uhakika wa maisha na maendeleo katika sayari hii ambayo ni nyumba yetu sote viko mahali salama.
Kwanza ni pale nilipoingia Mtaa wa Roboti katika Bustani ya Dunia ya Xinghe kwenye Mtaa wa Bantin, eneo la Longgang. Pamoja na maendeleo makubwa ya mambo ya roboti na AI niliyoshuhudia, duka la kwanza la roboti la 6S duniani katika eneo hili, lilinipa mustakabali wa kipekee wa Shenzhen na China kwa ujumla, nakuhisi tayari ninaishi siku za baadaye.
Ndani ya duka hili sikuhisi kama duka la kawaida la vifaa vya kielektroniki. Roboti za maumbo ya binadamu zilikuwa zikisogea kila mahali, mbwa roboti zilikuwa zikifanya mazoezi, mikono ya roboti ilikuwa na pilika za kupika chakula. Huku mambo mengi kuanzia huduma za vinywaji, chakula na nyinginezo zikifanywa na roboti, nilijiona sasa niko kwenye ulimwengu maridhawa na usio wa kawaida. Hata chakula cha mchana nilichokula kwa mara ya kwanza nilihudumiwa na roboti.
Msingi mkuu wa duka hili ni kuwa jukwaa lenye kutilia mkazo kazi sita muhimu: Maonyesho, Mauzo, Mafunzo, Jamii, Suluhisho, na Uvumbuzi Unaoanza. Linavunja vikwazo vya uvumbuzi wa kiteknolojia, likiwapa watu binafsi, kampuni na wabunifu wa programu uungaji mkono wa mwanzo-hadi-mwisho kuanzia msukumo wa uvumbuzi hadi uzinduzi wa bidhaa.
Hapa unaweza kukodisha roboti kwa ajili ya tukio au maonyesho, au kuwa na moja iliyoundwa mahsusi kwa ajili ya kazi maalum - viwanda, biashara, matibabu, elimu, na hata matumizi ya nyumbani kama vile kusaidia kazi za dukani, kutengeneza kahawa, juisi na hata kufanya mambo yote yanayohusiana na usafi na mazoezi ya viungo.
Eneo hili kimya kimya linaandika simulizi ya aina yake. Kampuni nyingi za mambo ya roboti na AI, ikiwemo ile yenye jina kubwa ya nchini China ya Unitree, ziko hapa. Mnyororo mzima wa viwanda - kuanzia sehemu muhimu na vihisi hadi programu na matumizi ya mwisho - umekusanyika katika sehemu moja inayoweza kufikika.
Baadaye nilielekea Bustani ya Ikolojia ya Nishati ya Longgang, moja ya mtambo mmoja mkubwa zaidi duniani wa kuchakata taka hadi kuwa nishati, ikiwa na uwezo wa kusindika tani 5,100 kila siku. Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa kwenye eneo la mradi, bustani hii imeundwa kwa mistari sita ya mashine za kuchakata taka kwa uwezo wa tani 850 kwa siku kwa kila moja.
Eneo hili kwa kutokea nje halionekani kama mtambo tu wa taka. Usanifu wake wenyewe ni uvumbuzi tosha. Ni jengo kubwa la mviringo la rangi ya chungwa lililozungukwa na vilima huku vifuniko vya chuma vikishikilia nafasi nyepesi na za kijani pande zote. Wenyeji huichukulia kama bustani ya matembezi.
Ndani yake, uwezo wake ni usio na kifani: hushughulikia takriban robo ya taka zote za majumbani za Shenzhen kila siku—maelfu ya tani—kupitia usindikaji kwenye joto kali unageuza taka kuwa umeme. Umeme unaozalishwa hapa ni mwingi, kuweza kutosha kufidia sehemu kubwa ya mahitaji ya wilaya hii.
Kushuhudia maeneo haya yote mawili katika siku moja kumeniacha nikifikiria namna Mji wa Shenzhen unavyosokota teknolojia na ikolojia katika kitambaa cha mji. Yamenipa mistakabali miwili muhimu. Duka la roboti linaonesha jinsi uvumbuzi unavyoweza kupanuka na kuwafikia watu haraka zaidi, kufanya kila jambo kuwa rahisi. Bustani ya ikolojia ya nishati inaonesha jinsi miundombinu ya nishati inavyoweza kuhudumia mazingira na jamii kwa wakati mmoja.

Meli hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Cote d'Ivoire kutekeleza jukumu la matibabu

Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China

Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China

Mabaki ya vivutio vya kihistoria vya Safari Ndefu mkoani Sichuan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
