Lugha Nyingine
Kiasi cha mizigo inayosafirishwa kupitia Mfereji wa Pinglu mkoani Guangxi, China, kimezidi tani milioni moja
Tangu Mfereji wa Pinglu ulipoanza kutumika tarehe 16 Septemba, kiasi cha mizigo inayosafirishwa kupitia mfereji huo kimezidi tani milioni moja.
Mfereji huu wenye urefu wa kilomita 134.2 unatoka Nanning, mji mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, hadi Ghuba ya Beibu, ambayo ni lango la bahari lililo karibu zaidi kwa maeneo ya kusini-magharibi mwa China.
Mfereji huu unafuata Ushoroba Mpya wa Biashara ya Kimataifa ya Baharini na Nchi Kavu wa Magharibi mwa China, ambao ni njia ya biashara ya kimkakati inayounganisha maeneo ya ndani ya China na ASEAN pamoja na masoko mengine duniani. Mfereji wa Pinglu ni mradi wa kwanza wa mfereji unaounganisha mito na bahari uliopangwa na kuratibiwa kwenye ngazi ya serikali tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China mwaka 1949.

Meli hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Cote d'Ivoire kutekeleza jukumu la matibabu

Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China

Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China

Mabaki ya vivutio vya kihistoria vya Safari Ndefu mkoani Sichuan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
