Lugha Nyingine
Idadi ya Wanunuzi wa Kigeni katika Kipindi cha Kwanza cha Maonyesho ya Canton yafikia rekodi mpya ya juu (2)
Shughuli ya ana kwa ana ya kipindi cha kwanza cha Maonyesho ya 140 ya Uagizaji na Uuzaji wa Bidhaa ya China (Maonyesho ya Canton) zimemaliza jana Jumatatu, na idadi ya wanunuzi wa kigeni waliotokea ikifikia rekodi mpya ya juu zaidi katika historia yake.
Hadi Jumatatu, wanunuzi wa kigeni 189,000 kutoka nchi na maeneo 214 walikuwa wameshiriki kwenye maonesho hayo, idadi ambayo iliongezeka kwa asilimia 13.3 ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha maonesho hayo yaliyopita.
Mwandalizi wa maonyesho hayo, Kituo cha Biashara na Nje ya China, kilisema idadi hii ya washiriki iliyoweka rekodi mpya inaonyesha hali yenye nguvu ya uthabiti na uhai ya biashara na nje ya China.
Kipindi hicho cha kwanza kilikuwa na kaulimbiu ya “Utengenezaji wa Kisasa”, na ukubwa wa eneo la maonesho ya bidhaa umefikia mita za mraba 520,000, ambapo kuna mabanda zaidi ya 25,000 ya maonesho, na makampuni na viwanda zaidi ya 12,000 vimeshiriki kwenye maonesho hayo.
Maonyesho hayo yatafanyika kwa vipindi vitatu, ambavyo vyote vitafanyika katika Mji wa Guangzhou wa Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, maonesho hayo yataendelea hadi tarehe 4 Novemba. Kipindi cha pili cha kaulimbiu ya “Maisha ya Sifa Bora Nyumbani”, na kitafanyika kuanzia tarehe 23 hadi 27, Oktoba.

Meli hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Cote d'Ivoire kutekeleza jukumu la matibabu

Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China

Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China

Mabaki ya vivutio vya kihistoria vya Safari Ndefu mkoani Sichuan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
