Lugha Nyingine
Timu ya madaktari wa China yatoa huduma ya bure ya matibabu kusini mwa Cameroon (2)
Timu ya 25 ya madaktari wa China nchini Cameroon imetoa huduma ya bure ya matibabu huko Meyomessala, mkoa wa Kusini nchini humo kuanzia Alhamis iliyopita hadi Jumamosi.
Wakati wa shughuli hiyo ya siku tatu, karibu wagonjwa 1,000 walipata huduma ya bure ya ushauri na tiba kwa magonjwa ya aina mbalimbali, na huduma hizo zilikuwa pamoja na tiba kwa magonjwa ya ndani, upasuaji, tiba kwa magonjwa ya wanawake, na tiba ya jadi ya sindano.
Ijumaa iliyopita, Waziri wa Afya ya Umma wa Cameroon Manaouda Malachie alitembelea eneo ambako shughuli ilifanyika na kusifu kazi ya timu ya madaktari wa China nchini Cameroon.
Madaktari hao pia walichangia dawa mbalimbali kwa hospitali ya huko.

Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China

Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China

Mabaki ya vivutio vya kihistoria vya Safari Ndefu mkoani Sichuan, China

Mwonekano wa kisiwa cha Liugong la eneo la mji Weihai mkoani Shandong China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
