Jukwaa la Beijing lajadili changamoto za kupambana na ugaidi zinazotokana na teknolojia za AI (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 16, 2026
Jukwaa la Beijing lajadili changamoto za kupambana na ugaidi zinazotokana na teknolojia za AI
Washiriki wakichangamana na roboti kwenye Jukwaa la Kimataifa la Ukuta Mkuu 2026 juu ya Kupambana na Ugaidi lililofanyika Beijing, Oktoba 14, 2026. (Picha na Ze Fangningchen/Xinhua)

BEIJING - Jukwaa la Kimataifa la Ukuta Mkuu-2026 juu ya Kupambana na Ugaidi limemalizika mjini Beijing jana Alhamisi, ambapo wataalamu na wahusika wa mstari wa mbele zaidi ya 320 kutoka nchi 62 na mashirika ya kimataifa wakijadili changamoto za kupambana na ugaidi, ikiwa ni pamoja na matatizo yanayotokana na maendeleo ya teknolojia kuhusu uendeshaji bila binadamu na za AI.

Wakati wa jukwaa hilo la siku tatu, washiriki walijadili hali ya ugaidi, kutafuta njia za utatuzi na kukabiliana na changamoto za pamoja, kubadilishana uzoefu wa vitendo na uwezekano wa kufanya ushirikiano wa kimataifa.

Washiriki wameeleza kuwa maendeleo ya haraka ya teknolojia kuhusu uendeshaji bila binadamu na za AI yamefanya shughuli za kigaidi kuzidi kuwa na hali ya kujificha na kuongeza uharibifu zaidi, kwani mbinu mpya zinatumika kutekeleza vitendo vya ugaidi na mabavu.

Wamesema mbinu za kawaida ambazo zinategemea nchi moja moja kufanya vitendo pekee yao na kuchukua hatua za kuzuia na kudhibiti kwa upweke zinazidi kuwa njia zinazoshindwa zaidi kukabiliana na matishio ya ugaidi yanayoibuka yaliyo ya kuvuka mikapa, ya kujificha na ya kuwezeshwa na nguvu ya teknolojia za AI.

Washiriki wamesema kupambana na ugaidi kunahitaji nchi mbalimbali kuendana na maendeleo ya teknolojia kuhusu uendeshaji bila binadamu na za AI, kuimarisha uwezo wao wa kupambana na ugaidi, na kufanya juhudi za pamoja za kuanzisha na kukamilisha mifumo ya ushirikiano wa kimataifa ya kuzuia na kupambana na ugaidi.

Mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa jukwaa hilo la Ukuta Mkuu. Tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2016, Jeshi la Askari Polisi la China limekuwa likiandaa jukwaa hilo kwa mara 6.

Shughuli za Jukwaa hilo la mwaka huu ziliweka mkazo katika kufuatilia mazingira yanayobadilika kila mara, maadui wanaojiendeleza hatua kwa hatua pamoja na maendeleo ya teknolojia, na pia kufanya majadiliano kuhusu athari ya AI kwa juhudi za kuzuia na kupambana na ugaidi.

Majadiliano yalipangwa katika majukwaa ya ngazi ya juu, ya kitaaluma na ya mada maalumu, na kuandaa jukwaa la mazungumzo la pande zote na la ngazi mbalimbali linalohusisha mambo ya kimkakati, ya uendeshaji, na mbinu za mapambano.

China ambayo ni mshiriki na mtoaji mchango muhimu katika mapambano ya kimataifa dhidi ya ugaidi, imeshiriki katika ushirikiano wa kivitendo na nchi nyingine katika kubadilishana upelelezi, udhibiti wa mipaka, uchunguzi wa kesi na kukusanya mitaji kwa mapambano dhidi ya ugaidi.Pia imeandaa vipindi vya mafunzo na semina ili kuchangia uzoefu wake na jumuiya ya kimataifa, na kusaidia kuimarisha uwezo wa kupambana na ugaidi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha