Lugha Nyingine
Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 15, 2026
![]() |
| Wasanii wakicheza ngoma ya simba kwenye hafla ya kufunguliwa kwa Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma, Macao, kusini mwa China, tarehe 13 Oktoba 2026. (Xinhua/Cheong Kam Ka) |
Katika mitaa ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao (SAR) wa China Jumanne wiki hii watu walifanya maandamano wakibeba Sanamu ya Mazu, Mungu wa kike wa baharini katika utamaduni wa China, wakati Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lilipofunguliwa.
Hafla ya kufunguliwa kwa tamasha hilo iliyofanyika kwenye Kijiji cha Utamaduni cha A-Ma ilifuatiwa na mila za jadi za kumheshimu Mungu huyo wa kike, na maandamano ya mitaani yalifanyika wakati wa mchana.
Tamasha hilo linaonesha ufundi wa jadi wa kazi za sanaa za Mkoa wa Fujian, mashariki mwa China. Maonesho ambayo yalifunguliwa Jumatatu yameonesha kazi 56 za sanaa, zikiwemo vyombo vya kauri, michongo ya mbao, na vyombo vilivyopakwa vanishi ya asili ya jadi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




