Njia mpya ya usafiri wa ndege kati ya China na Ethiopia yazinduliwa (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 14, 2026
Njia mpya ya usafiri wa ndege kati ya China na Ethiopia yazinduliwa
Abiria wa ndege inayoendeshwa na shirika la ndege la China Southern wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Addis Ababa Bole jijini Addis Ababa, Oktoba 12, 2026. (Xinhua/Geng Xinning)

ADDIS ABABA - Ndege ya shirika la ndege la China Southern imewasili nchini Ethiopia jana Jumatatu, hali ambayo ilionesha usafiri wa kwanza wa ndege ya abiria umefanikiwa kwenye njia mpya kati ya China na Ethiopia iliyoanzishwa na shirika hilo la ndege la China.

Ndege hiyo, iliyokuwa imebeba abiria zaidi ya 200, ilipokelewa kwa saluti ya jadi ya kupulizwa maji wakati ikiwasili.

"Sisi ni kundi la watalii kutoka Guangzhou, lenye watu 20. Tumehudumiwa na usafiri wa ndege wa kwanza wa Shirika la Ndege la Nanfang la China kuja Addis Ababa. Tuna furaha sana, na pia tumepata kumbukumbu nyingi ambazo hatutaweza kuzisahau," amesema Zhu Binghong, mwongozaji wa kundi hilo la watalii.

Zhu amejulisha kuwa, watalii wa kundi hilo watakuwa Ethiopia kwa siku tisa, ambapo watatembelea mji mkuu na sehemu za makabila ya Kusini mwa Ethiopia.

Usafiri wa ndege hiyo ya abiria utafanyika mara mbili kwa wiki, siku za Jumatatu na Ijumaa, kutoka mji wa Guangzhou wa kusini mwa China na kupita mji wa Changsha wa katikati mwa China, halafu kuelekea mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Kutokana na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na mawasiliano kati ya watu wa China na Afrika vinavyoendelea kukua, shirika hilo la ndege la China limesema litaendelea kupanua njia za usafiri wa ndege kati ya mabara mbalimbali na kuongeza mawasiliano ya anga kati ya China na Afrika ili kuhimiza mafungamano ya usafiri kati ya pande mbili za China na Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha