Watalii wa kigeni wamiminika Longji ili kujionea na kuyaishi maisha ya kijadi ya vijijini China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 12, 2026
Watalii wa kigeni wamiminika Longji ili kujionea na kuyaishi maisha ya kijadi ya vijijini China
Mwanakijiji akitembea kuelekea shambani katika Kijiji cha Longji cha Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Wage ya Longsheng katika Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, Agosti 16, 2026. (Xinhua/Cao Yiming)

Mashamba ya mpunga ya Longji yaliyopangwa kwa mtindo wa ngazi (terraces) katika Kijiji cha Longji cha Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Wage ya Longsheng katika Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China ni kivutio maarufu kwa watalii wanaotaka kujionea na kuyahisi maisha ya kijadi ya vijijini China. Katika kijiji hicho, wanaishi watu wengi zaidi wa kabila la Wazhuang, kijijini humo kuna nyumba za mbao za kijadi zilizojengwa katikati ya mashamba hayo ya ngazi na kinadumisha mtindo wa utamaduni wa kipekee wa kabila la Wazhuang.

Kijiji hicho kikifuata desturi zake za kilimo cha mpunga zenye historia ya miaka mia kadhaa kimefunganisha mali ya urithi wa kitamaduni na shughuli za utalii, kinaandaa shughuli mbalimbali za kupanda milima, kutembelea kijijini, kujionea na kushiriki shughuli za kilimo na utengenezaji wa kazi za mikono. Shughuli hizo zimevutia watalii wengi wa kigeni wenye shauku ya kujionea na kufurahia mandhari nzuri kushiriki kwenye shughuli za kilimo cha kijadi cha mpunga na shughuli za utamaduni wa kabila hilo la China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha