Reli za China zafikia kilele cha pilika za usafiri wa abiria baada ya shughuli za utalii wakati wa siku za mapumziko (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 08, 2026
Reli za China zafikia kilele cha pilika za usafiri wa abiria baada ya shughuli za utalii wakati wa siku za mapumziko
Abiria wakionekana ndani ya ukumbi wa kusubiria wa Stesheni ya Reli ya Hongqiao ya Shanghai mashariki mwa China, tarehe 7 Oktoba 2026. (Xinhua/Ding Ting)

BEIJING - Reli za China jana jumatano zimefikia kilele cha pilika nyingi za kuwasafirisha watu kurudi nyumbani baada ya utalii wa siku za mapumziko, imekadiriwa kuwa safari za abiria zilifikia milioni 24.15 siku hiyo ambayo ni siku ya mwisho ya mapumziko ya Sikukuu ya Taifa, kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri na mawimbi ya shughuli za utalii katika sehemu mbalimbali nchini China.

Kampuni ya Kundi la Shirika la Reli la China imesema jumla ya treni 2,449 za ziada za abiria zilikuwa zimepangwa kwa ajili ya siku hiyo ya Jumatano ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji.

Kampuni hiyo imesema siku ya Jumanne iliyopita, reli za kote nchini China zilihudumia safari za abiria milioni 21.6, na hii ni siku ya tatu mfululizo yenye safari za abiria zaidi ya milioni 20.

Beijing, Guangzhou, Chengdu, Xi'an, Wuhan, Hangzhou, Chongqing na Shanghai ni miji iliyokuwa na pilika nyingi zaidi za kuondoka na kuwasili kwa abiria, wakati huohuo idadi ya abiria ilikuwa kubwa zaidi kwenye njia za usafiri za Beijing-Shanghai, Wuhan-Shanghai, Wuhan-Shenzhen na Xi'an-Chengdu.

Mamlaka za reli katika sehemu mbalimbali nchini China ziliongeza usafiri wa treni na kupanua shughuli za usafiri wa usiku ili kuwezesha pilika nyingi za usafari wa watu wa kurudi nyumbani, kutokana na soko la utalii la China kuendelea kushamiri wakati wa siku saba za mapumziko, ambapo shughuli za utalii katika wilaya mbalimbali na matumizi ya watu wakati wa usiku vimekuwa mawimbi zaidi.

Watalii wengi sasa wanapenda zaidi kwenda sehemu zilizoko mbali na miji mikubwa na zenye mazingira mazuri tulivu ili kufanya utalii polepole na kujionea mengi zaidi ya kuvutia, ndiyo maana sehemu mbalimbali za wilaya nchini zimependelewa zaidi na watalii wengi.Kuanzia wilaya ya pwani ya Lingshui katika Mkoa wa Hainan kusini mwa China hadi Mohe, mji wa wilaya kwenye mpaka wa kaskazini mwa China, maeneo madogo zaidi yanavutia watalii kwa mazingira yao ya kipekee.

Wakati huo huo, matumizi ya watu wakati wa usiku yalistawi katika miji mingi, ambapo maonyesho ya kitamaduni, masoko ya usiku, maonyesho ya mvuto wa mwanga wa taa na maonyesho ya vyakula yakiwafanya watalii wang’ang’anie zaidi huko na kuwapa raha na starehe zaidi wakati wa siku za mapumziko.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha