Lugha Nyingine
"Kiwanda cha Siku za Baadaye" cha kuunda meli Dalian, kaskazini mashari mwa China
![]() |
| Picha iliyopigwa Septemba 1, 2026 ikionesha mandhari ya eneo la Viwanda Vizito la Hengli la Dalian, mkoani Liaoning, kaskazini mashariki mwa China. (Xinhua) |
DALIAN - Eneo la Viwanda Vizito la Hengli liko katika Eneo la Kiuchumi la Kisiwa cha Changxing la Mji wa Dalian, mkoani Liaoning, kaskazini mashariki mwa China, lilianzisha "Kiwanda cha Baharini," mwanzoni mwa mwaka 2023, eneo hilo ni kituo cha uundaji meli bila kuleta uchafuzi kwa mazingira.
Kiwanda chake cha "Siku za Baadaye" kilianza kuendeshwa mwanzoni mwa mwaka 2025, kinabobea katika uundaji wa meli bila kuleta uchafuzi zenye nyongeza za thamani, na meli hizo zikiwa ni pamoja na meli kubwa kupita kiasi za kubeba mafuta, meli kubwa za kupita kiasi za kubeba gesi ya kimiminika hadi meli kubwa za kupita kiasi za kubeba makontena, pamoja na zana na vifaa vya hali ya juu vya uhandisi wa baharini.
Katika eneo hilo la viwanda vizito, teknolojia mpya za kisasa kama vile za kutumia roboti za kuchomelea, kukata kiotomatiki, na uwekaji alama kwenye chuma kiotomatiki zinatumika sana. Na zana na vifaa mbalimbali vya kukusanya data za viwandani vimewekwa kwenye majukwaa ya kujenga meli, karakana na magati.
Kwa kutumia teknolojia za hali ya juu katika kukusanya data za viwanda, teknolojia za kuhisi kwa kutumia IoT na mitandao ya kibinafsi ya 5G, kiwanda hicho kizima kimetimiza matumizi ya kidigitali ya mambo yanayohusiana na uzalishaji vilevile usimamizi wa uendeshaji ulio wa makini kabisa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




