Huduma za Dunia Nzima, Ustawi wa Pamoja: Maonesho ya Biashara ya Huduma ya China 2026 yafunguliwa (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 10, 2026
Huduma za Dunia Nzima, Ustawi wa Pamoja: Maonesho ya Biashara ya Huduma ya China 2026 yafunguliwa
Watu wakizungumza kwenye banda la Norway, nchi mgeni wa heshima wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China (CIFTIS) 2026, Beijing, Septemba 9, 2026. (Xinhua/Zhang Xiaoyu)

BEIJING - Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China 2026 (CIFTIS) yamefunguliwa rasmi Jumatano mjini Beijing, wakati huu ambapo China inaongeza juhudi za kupanua ufunguaji mlango katika biashara ya huduma mwanzoni mwa kipindi cha Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030).

Maonesho hayo yanafanyika hadi Septemba 13 kwenye Bustani ya Shougang, ambayo iliyokuwa sehemu ya viwanda vya zamani, ambapo pia ilikuwa mahali pa majengo ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022, yamevutia washiriki kutoka nchi, maeneo na mashirika ya kimataifa 90, na kampuni zaidi ya 1,800 zimeshiriki kwenye maonesho hayo.

Maonesho hayo ya mwaka huu yenye kaulimbiu ya "Huduma za Dunia Nzima, Ustawi wa Pamoja," yanashirikisha Mkutano wa Kilele wa Biashara ya Huduma ya Dunia Nzima, ulioandaliwa kwa mara ya kwanza pamoja na Shirika la Haki Miliki ya Ubunifu Duniani. Mfululizo wa majukwaa na shughuli za kukutanisha wafanyabiashara pia zitafanyika wakati wa maonesho hayo.

Eneo kuu la maonyesho hayo pia linaonyesha mifano zaidi ya 140 ya uvumbuzi inayohusu aina 12 za biashara ya huduma, ikiwa ni pamoja na AI, mifano mikubwa ya lugha, na mawakala wa akili, hali ambayo inawawezesha watu waone mwelekeo wa maendeleo ya shughuli za huduma nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha