Wanafunzi wa Hong Kong na Macao wazungumza na wanaanga wa Shenzhou-23 waliopo anga ya juu kwenye "Darasa la Tiangong" (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 10, 2026
Wanafunzi wa Hong Kong na Macao wazungumza na wanaanga wa Shenzhou-23 waliopo anga ya juu kwenye
John Lee, afisa mtendaji mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR), na wanafunzi wakihudhuria mhadhara wa moja kwa moja wa anga ya juu wa "Darasa la Tiangong" Kipindi Mahsusi kwa ajili ya Hong Kong na Macao wakiwa kwenye Hong Kong, kusini mwa China, Septemba 9, 2026. (Picha na Lui Sui Wai/Xinhua)

HONG KONG – Kipindi cha "Darasa la Tiangong" Mahsusi kwa Hong Kong na Macao kimefanyika kwa wakati mmoja huko Hong Kong na Macao jana Jumatano asubuhi, wakati wanaanga watatu wa China wa chombo cha Shenzhou-23 wanaofanya jukumu la anga ya juu kwenye kituo cha anga ya juu cha Tiangong walipotoa mhadhara wa moja kwa moja kutoka anga ya juu kwa wanafunzi.

Kamanda wa jukumu la chombo cha Shenzhou-23 Zhu Yangzhu, mwanaanga Zhang Zhiyuan na mtaalamu wa kwanza wa vifaa na majaribio ya anga ya juu wa Hong Kong Li Jiaying, au Lai Ka-ying katika lugha ya Kikantoni, walitoa somo wazi la sayansi la kubadilishana maoni kwa vijana wa Hong Kong na Macao.

Shughuli hiyo iliandaliwa kwa pamoja na serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR), serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao (SAR) na Shirika la Anga ya Juu wa China, huku darasa kuu likiwa limewekwa katika shule ambako Lai aliwahi kusoma, Chuo cha Umma cha Ukumbusho wa Ho Chuen Yiu cha Tsuen Wan mjini Hong Kong.

Jumla ya wanafunzi 160 wa Hong Kong na wanafunzi 50 wa Macao walihudhuria kwenye ukumbi mkuu ana kwa ana, wakijumuika na wakuu wa shule, walimu, wawakilishi wa vijana, na wataalamu wa teknolojia kutoka miji yote hiyo miwili.

Serikali ya HKSAR na serikali ya Macao SAR pia zilipanga walimu na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kutazama matangazo hayo ya moja kwa moja shuleni kwa wakati mmoja.

Kwenye kipindi hicho, wanaanga hao watatu walionyesha majaribio ya kisayansi katika mazingira ya kipekee ya anga ya juu kwa wakati halisi na kuonesha hali halisi ya maisha ya kila siku ndani ya kituo cha anga ya juu. Walifanya mfululizo wa matukio ya kuonesha sayansi, ikiwa ni pamoja na kuoka keki kwenye jiko la anga ya juu, kukunja taulo iliyolowa maji, na kutunza bustani ya mboga za majani kwenye anga ya juu.

Wakati wote wa mhadhara huo, wanaanga walijibu maswali kutoka kwa wanafunzi kuhusu sayansi ya anga ya juu na maisha ya wanaanga kwenye obiti.

John Lee, afisa mtendaji mkuu wa HKSAR, alimuuliza Lai kama alikuwa amepokea barua zilizotumwa na wanafunzi. Katika jibu lake, Lai alisema alikuwa amesoma kila barua kutoka nyumbani, akiahidi kuheshimu imani yao na kufanya juhudi zote kukamilisha jukumu lake hilo kwenye obiti. Ameongeza kuwa safari yake hiyo ya anga ya juu inaakisi uungaji mkono mkubwa wa serikali kuu kwa Hong Kong.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha