Timu ya matibabu ya China yatoa huduma za matibabu bila malipo nchini Sierra Leone (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 08, 2026
Timu ya matibabu ya China yatoa huduma za matibabu bila malipo nchini Sierra Leone
Madaktari wa kundi la 27 la timu ya madaktari ya China nchini Sierra Leone wakiwapima wakazi wenyeji shinikizo la damu kwenye shughuli ya afya kwa jamii bila malipo, Freetown, Sierra Leone, Septemba 5, 2026. (Kundi la 27 la timu ya matibabu ya China nchini Sierra Leone/kupitia Xinhua)

FREETOWN - Kundi la 27 la timu ya matibabu ya China nchini Sierra Leone limetoa huduma za matibabu zaidi ya 300 bila malipo kwenye shughuli ya pamoja ya kutoa huduma za afya kwa jamii kwenye Kituo cha Afya cha Wilberforce mjini Freetown chini ya mpango wa China wa "Timu 100 za Madaktari katika Vijiji 1,000".

Shughuli hiyo ya nusu siku Jumamosi iliwaleta pamoja timu ya taaluma mbalimbali ya wataalamu wa afya wa China na Sierra Leone kutoa huduma za matibabu ya ndani, upasuaji, magonjwa ya wanawake, Tiba ya Jadi ya Kichina, magonjwa ya macho na masikio, pua na koo.

Wataalamu wabobezi waliwafanyia tathmini na kutibu wagonjwa wenye shinikizo la damu, magonjwa ya utumbo na ya kuambukizwa, ugonjwa wa kuchakaa kwa viungo, pamoja na matatizo yanayohusiana na kazi, na matatizo mengine yanayohitaji huduma za upasuaji, wakati huohuo walitoa dawa na ushauri wa afya.

Wahudumu wa afya na watu wa kujitolea wenyeji waliunga mkono usajili wa wagonjwa, uchunguzi wa awali na kutafsiri katika kipindi chote cha huduma hiyo ya matibabu bila malipo.

Osman Kamar, afisa mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Wilberforce, ametoa shukrani kwa mpango huo, akiuelezea kuwa ni mchango halisi kwa afya ya jamii na ametoa wito kwa timu ya matibabu ya China kufanya ziara kama hizi mara kwa mara siku zijazo.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha