Chama cha AfD cha mrengo wa kulia kabisa chapata ushindi kwenye uchaguzi wa jimbo wa Ujerumani (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 07, 2026
Chama cha AfD cha mrengo wa kulia kabisa chapata ushindi kwenye uchaguzi wa jimbo wa Ujerumani
Wapiga kura wakipiga kura kwenye kituo cha kupigia kura, Magdeburg, Ujerumani, Septemba 6, 2026. (Xinhua/Zhang Haofu)

MAGDEBURG, Ujerumani - Matokeo ya kura za maoni za wapiga kura waliotoka vituoni yaliyotolewa na shirika la utangazaji la umma la Ujerumani ARD yameonesha kuwa, Chama cha Chaguo Lingine cha Ujerumani (Alternative for Germany, AfD), ambacho ni chama cha mrengo wa kulia kabisa nchini Ujerumani kimeshinda uchaguzi wa jimbo wa jana Jumapili katika Jimbo la Saxony-Anhalt kwa rekodi ya kupata asilimia 44.4 ya kura zilizopigwa.

Chama cha Christian Democratic Union (CDU), kinachoongozwa na Sven Schulze, kiongozi wa jimbo aliye madarakani sasa kimepata pigo kubwa, na kura zake za maoni zimeshuka hadi asilimia 18.4, kutoka asilimia 37.1 mwaka 2021.

Inaonesha kuwa, Chama hicho cha mrengo wa Kushoto kimeshika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 9.3 ya kura zilizopigwa, kikifuatiwa na Greens kwa asilimia 8.7 na Chama cha Social Democratic (SPD) kwa asilimia 8.4.

Muungano mpya wa Sahra Wagenknecht (BSW) ulioundwa hivi karibuni umepata asilimia 5 ya kura zinazouwezesha kuingia kwenye bunge la jimbo hilo, wakati Free Democratic Party (FDP) ambacho ni rafiki kwa biashara kikishindwa kuingia bungeni kwa kupata asilimia 2.2 tu za kura zilizopigwa.

Akikubali kushindwa kwake, Schulze amekiri ushindi dhahiri wa AfD, wakati huohuo amehimiza viongozi wa kisiasa kote Ujerumani kusikiliza kwa makini maoni waliyotoa wapiga kura.

Jijini Berlin, mkuu wa ofisi ya Chansela Nina Warken ameyaita matokeo hayo ya uchaguzi kuwa ni "wakati wa mabadiliko makubwa" kwa CDU, akiyaelezea kwenye Televisheni ya ZDF kuwa ni "matokeo magumu sana, sana." Warken pia amesisitiza kwamba serikali kuu itasukuma mbele kithabiti ajenda yake ya mageuzi iliyopangwa.

Kwenye bunge la jimbo hilo lenye viti 83, chama cha AfD kinakadiriwa kupata viti 39, bado kuna upungufu wa viti vitatu vinavyohitajika kwa kukiwezesha kuwa chama chenye viti vingi kabisa kinachofanya utawala peke yake.

Mgombea mkuu wa jimbo hilo wa AfD mwenye umri wa miaka 35, Ulrich Siegmund, ameyasifu matokeo hayo, akitangaza kwamba "wananchi wametoa ishara wazi."

Akihojiwa na ARD, Siegmund pia amesema alibadilisha kwa kiasi fulani msimamo wake wa kabla ya uchaguzi wa kutafuta wadhifa kwa kupitia chama chake kujipatia viti vingi kabisa, na amesema kuwa chama chake sasa kinapenda kufanya ushirikiano na chama kingine wa kuongoza serikali ya jimbo.

Hata hivyo, vyama vingine vyote vikuu vimekuwa vikiondoa uwezekano mara kwa mara wa kuingia katika ushirikiano wa kutawala na chama cha AfD. Hivi sasa hali ya namna gani ya kuundwa kwa serikali ya jimbo bado haijaonekana wazi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha