Waokoaji zaidi ya 2,500 wametumwa kwenye forodha ya mpakani iliyoathiriwa na maporomoko ya udongo na mawe mkoani Xizang, China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 07, 2026
Waokoaji zaidi ya 2,500 wametumwa kwenye forodha ya mpakani iliyoathiriwa na maporomoko ya udongo na mawe mkoani Xizang, China
Waokoaji wakifanya kazi kwenye eneo lililoathiriwa zaidi la Forodha ya Gyirong iliyokumbwa na maporomoko ya udongo na mawe, Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China, Septemba 6, 2026. (Xinhua/Tenzin Nyida)

GYIRONG, Xizang - China imepeleka waokoaji zaidi ya 2,500 baada ya maporomoko ya udongo na maweudongo na mawe kuikumba Forodha ya Gyirong kwenye mpaka wa China na Nepal katika Mkoa unaojiendesha wa Xizang kusini magharibi mwa China, Agosti 26, kituo cha uratibu wa kukabiliana na dharura na uokoaji ya China yamesema katika taarifa ya jana Jumapili.

Maporomoko hayo ya udongo na mawe yaliyosababishwa na kuanguka kwa ghafla kwa barafu ya mlimani ulioko kwenye mwinuko mrefu nchini Nepal, yamesababisha watu 43 kufariki na wengine 519 kutojulikana walipo kwenye forodha hiyo ya mpakani hadi kufikia saa 12 jioni juzi Jumamosi, maafisa wameuambia mkutano na waandishi wa habari.

Maafisa hao wamesema hadi kufikia saa 12 hiyo ya jioni siku ya Jumamosi, watu zaidi ya 2,500 na magari zaidi ya 500 walikuwa wametumwa kujiunga na shughuli za uokoaji, na zaidi ya safari 1,000 za droni zilikuwa zimedondosha tani 5.43 za vifaa kwa njia ya anga.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha