Lugha Nyingine
Umeme warejeshwa kwenye forodha ya mpakani iliyoathiriwa na maporomoko ya matope mkoani Xizang, China (4)
![]() |
| Wafanyakazi wakifunga nyaya za umeme kwenye eneo lililoathiriwa zaidi la Forodha ya Gyirong katika Mkoa unaojiendesha wa Xizang, kusini-magharibi mwa China, Septemba 3, 2026. (Xinhua/Jigme Dorje) |
BEIJING – Usambazaji umeme umerejeshwa katika eneo lililoathirika zaidi la Forodha ya Gyirong katika Mkoa unaojiendesha wa Xizang kusini-magharibi mwa China, Kampuni ya Gridi ya Taifa ya China imesema jana Alhamisi.
Kampuni hiyo imesema licha ya hatari kama vile maporomoko ya ardhi na kuanguka mara kwa mara kwa miamba, wafanyakazi wa mstari wa mbele wamefanya kazi usiku na mchana kurejesha njia za muda za kusambaza umeme katika eneo hilo lililoathiriwa zaidi la forodha hiyo saa 2 usiku jana Alhamisi.
Kwenye eneo hilo lililoathiriwa zaidi, jumla ya waokoaji 336 wamefanya raundi nyingi za utafutaji wa kina katika kila sehemu, wakihakikisha wamefika na kukagua kila sehemu.
Ili kusaidia zaidi juhudi za uokoaji, Wizara ya Usimamizi wa Dharura ya China, kwa kushirikiana na Wizara ya Uchukuzi ya China, zimetuma vifaa vya kuimarisha barabara na mitambo ya kunyanyua mizigo mizito katika eneo hilo.
Maporomoko hayo ya udongo na mawe ya mfululizo na kusonga kwa kasi, yaliyosababishwa na kuanguka kwa barafu za mlimani nchini Nepal, yaliikumba Forodha ya Gyirong Agosti 26, na kusababisha vifo vya watu 21 na kuwaacha wengine 541 wakiwa hawajulikani walipo hadi kufikia Jumatano adhuhuri.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




