Lugha Nyingine
Kimbunga Saudel chatua kwa mara ya tatu kando ya pwani ya mashariki mwa China
FUZHOU - Kimbunga Saudel, kimbunga cha 18 mwaka 2026 kuikumba China, kimetua kwa mara ya tatu mashariki mwa China jana Alhamisi asubuhi, na kusababisha makumi ya maelfu ya watu kuhamishwa huku kukiwa na tahadhari za upepo mkali na mvua kubwa.
Awali, kimbunga hicho kilitua mara mbili kando ya pwani ya Mkoa wa Zhejiang, pia uko mashariki mwa China, Agosti 28, na kusababisha uhamishaji wa mamia ya maelfu ya watu katika sehemu mbalimbali za mashariki mwa nchi hiyo.
Mamlaka husika mkoani Fujian zilikuwa zimehamisha watu zaidi ya 83,000 kufikia saa 1 asubuhi jana Alhamisi huku mvua kubwa ikinyesha katika sehemu za mkoa huo.
Mvua hiyo kubwa imesababisha kusimamishwa kwa shughuli za kazi, biashara na masomo shuleni katika sehemu za mji huo wa Zhangzhou. Shule pia zimefungwa katika miji mingine mkoani Fujian ikiwemo Fuzhou, Quanzhou na Ningde, mamlaka za mkoa huo zimesema.
Kufikia saa 1 asubuhi, sehemu nane za barabara kuu zilikuwa zimefungwa, huduma 657 za usafiri zimesimamishwa, kazi zimesitishwa katika maeneo 152 ya ujenzi, na vivutio vikubwa vya watalii zaidi ya 150 vimefungwa kote Fujian.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




