Lugha Nyingine
Watu 469 wafariki kwenye mafuriko yaliyotokea Nepal (4)
![]() |
| Watu wakifanya kazi ya uokoaji baada ya mafuriko makubwa ya ghafla huko Nuwakot, Nepal, Agosti 27, 2026. (Picha na Sulav Shrestha/Xinhua) |
KATHMANDU - Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Kupunguza Hatari za Maafa ya Nepal imesema kwamba miili ya watu 469 ilikuwa imeopolewa kutoka maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hadi kufikia leo Ijumaa asubuhi.
Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, hadi kufikia saa 4 usiku kwa saa za Nepal jana Alhamisi, jumla ya watu ambao hawakuwa wakipatikana kwenye mawasiliano ilikuwa 977.
Shughuli za uokoaji na utafutaji zinaendelea kwenye maeneo yaliyoathiriwa, huku mamlaka husika zikifanya kazi ya kuwapata watu wasiojulikana walipo na kuopoa miili zaidi.
Bodi ya Utalii ya Nepal imesema kwamba raia 31 wa kigeni wameokolewa kutoka maeneo yaliyoathiriwa.
Polisi wa Nepal wametoa wito kwa familia zote zilizoathiriwa na maafa hayo kwenda kituo cha polisi kilicho karibu na kuwasilisha taarifa na nyaraka husika za watu wasiojulikana walipo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




