Mkoa wa Heilongjiang, China waimarisha hatua za kuzuia mafuriko katika msimu mkuu wa mafuriko (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 07, 2026
Mkoa wa Heilongjiang, China waimarisha hatua za kuzuia mafuriko katika msimu mkuu wa mafuriko
Nyenzo za kuzuia mafuriko zikionekana katika Kijiji cha Hongqi cha Wilaya ya Lanxi, Mji wa Suihua, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Agosti 6, 2026. (Picha na Liu Huapeng/Xinhua)

Hatua za kuzuia mafuriko zimetekelezwa kote katika Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, ambao umeingia katika msimu wake mkuu wa mafuriko.

China imetenga yuan milioni 50 (dola karibu milioni 7.36 za Marekani) ambazo ni fedha kutoka serikali kuu ili kuunga mkono shughuli za kurejesha hali ya kawaida baada ya maafa katika Mkoa wa Heilongjiang uliokumbwa na mafuriko kaskazini mashariki, Kamati ya Kitaifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China (NDRC) ilisema Jumanne wiki hii.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha