Utamaduni wa karatasi ya Xuan wachochea ukuaji wa utalii katika Wilaya ya Jingxian, Anhui, China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 07, 2026
Utamaduni wa karatasi ya Xuan wachochea ukuaji wa utalii katika Wilaya ya Jingxian, Anhui, China
Mtalii wa kigeni akijifunza kutengeneza karatasi ya Xuan katika Wilaya ya Jingxian mkoani Anhui, mashariki mwa China, mnamo Julai 31, 2026. (Xinhua)

Karatasi ya Xuan ni karatasi iliyotengenezwa kwa makini sana kwa kupitia hatua kadha wa kadha ili kufikia ubora wa juu zaidi na matumizi yake ya muda mrefu zaidi. Kwa kawaida karatasi hiyo inatumika kwa kuandika maandiko ya maneno ya Kichina na kuchora picha za aina ya Kichina. Chimbuko lake lipo katika Wilaya ya Jingxian mkoani Anhui, mashariki mwa China, ambayo ilikuwa chini ya mamlaka ya Xuanzhou wakati wa Enzi ya Tang (618-907) -- na hivyo ndivyo jina la karatasi ya Xuan lilivyopatikana.

Kwa desturi za kijadi, karatasi hiyo inatengenezwa kwa nyasi ya mpunga na magome ya mti maalum unaopatikana nchini China pekee.

Katika miaka ya hivi karibuni, wilaya hiyo ya Jingxian imeingiza utamaduni wa karatasi ya Xuan kwenye ubunifu wa shughuli za utalii na utamaduni. Mbali na kutembelea kwenye maonyesho , watalii sasa wanaweza kujionea na kujaribu wao wenyewe ufundi wa hatua fulani wa kutengeneza karatasi hiyo ya Xuan baada ya kutazama kwa karibu mchakato mzima wa uzalishaji wa karatasi hiyo. Na watalii pia wanaweza kununua bidhaa mbalimbali za ubunifu wa kitamaduni na za ukumbusho wa wilaya hiyo.

Tokea mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, Wilaya ya Jingxian imepokea watalii milioni 3.2, ambayo ni ongezeko la asilimia 84.6 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, na kupata mapato ya shughuli za utalii ya yuan bilioni 1.657 (dola karibu milioni 245.5 za Marekani) katika kipindi hicho, ambayo ni ongezeko la asilimia 38.3 kuliko lile la mwaka jana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha