Lugha Nyingine
Mashine kubwa zaidi ya kuchimba mahandaki ya China yakamilisha uchimbaji wa handaki chini ya maji ya Mto Changjiang (2)
SHANGHAI - Mashine ya ngao ya kuchimba mahandaki yenye kipenyo kikubwa zaidi duniani, ikiundwa na China yenyewe kwa ajili ya miradi ya reli ya mwendo-kasi, imechimba shimo kwa mafanikio kupitia handaki la chini ya maji linalopitia Mto Changjiang jana ya Alhamisi.
Mafanikio hayo yataruhusu treni ya mwendo-kasi kuendeshwa chini ya Mto Changjiang kwa kasi ya kilomita 350 kwa saa katika usafiri mzima bila kupunguza mwendo kwa mara ya kwanza, ikionesha maendeleo makubwa katika teknolojia ya kuchimba mahandaki ya reli ya kuvuka mto nchini China.
Handaki hilo lenye urefu wa kilomita jumla ya 14.25 linalounganisha Eneo la Chongming la Mji wa Shanghai na Mji wa Taicang wa Mkoa jirani wa Jiangsu limejengwa kwa kufuata vigezo vya juu zaidi vya ujenzi kati ya miradi ya reli ya mwendo-kasi ya kuvuka mto nchini China, na pia ni moja kati ya miradi mikubwa yenye taabu za teknolojia katika ujenzi wa miundombinu ya aina yake.
Li Bin, mhandisi mkuu wa mradi huo wa handaki wa Kampuni ya Kundi la Mahandaki la Shirika la Reli la China amesema kuwa mashine hiyo ya ngao yenye urefu wa mita 148 ina uzito wa tani takriban 4,000 na ina kichwa kikubwa cha kukata cha mita 15.4, na imekuwa mashine ya kuchimba handaki yenye kipenyo kikubwa zaidi duniani kwa ujenzi wa reli ya mwendo-kasi.
Zana ya kuchimba handaki inayojiendesha kwa mara moja imechimba bila kukoma kwa umbali wa kilomita 11.325 chini ya maji ya Mto Changjiang, ikiweka rekodi mpya ya China kwa uchimbaji wa handaki ya mashine ya ngao ya ngazi ya mita 15.
Ujenzi wa handaki zima unakadiriwa kukamilika mwisho wa mwaka huu 2026. Mara tu mradi huo utakapoanza kutumika, utamaliza hali ya kutokuwa na njia ya reli ya mwendo-kasi kwenye eneo hilo la kisiwa la Chongming, na kupunguza muda wa kusafiri hadi kuwa dakika 17 tu kutoka Chongming kupitia Taicang hadi Stesheni ya Reli ya Baoshan ya Shanghai, hali ambayo itaboresha kwa kiasi kikubwa usafiri wa maeneo ya kikanda.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




