Merz asema Marekani haipaswi kuingilia uchaguzi wa Ujerumani (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 16, 2026
Merz asema Marekani haipaswi kuingilia uchaguzi wa Ujerumani
Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa serikali wa majira ya joto na waandishi wa habari, huko Berlin, Ujerumani, Julai 15, 2026. (Xinhua/Li Hanlin)

BERLIN - Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema kwamba hataki Marekani kuingilia uchaguzi wa Ujerumani.

Merz ameyasema hayo jana Jumatano kwenye mkutano wa mwaka wa serikali wa majira ya joto na waandishi wa habari alipoulizwa habari kuhusu mpango wa Marekani wa kuunga mkono makundi ya kisiasa na kiraia barani Ulaya, mpango unaokosolewa kwa sababu huenda unaweza kusaidia makundi kama yale yanayoendana kiitikadi na chama cha siasa cha mrengo-mkali wa kulia cha Ujerumani Alternative for Germany (AfD).

Merz amesema Ujerumani siku zote inajikwepa kuingilia uchaguzi wa Marekani. "Kinyume chake, mimi pia sitaki serikali ya Marekani au taasisi zilizo karibu nayo kuingilia uchaguzi wa Ujerumani," amesema.

Merz amedhihirisha kuwa kutoa mitaji kwa vyama vya kisiasa vya Ujerumani kutoka nje ya nchi ni kinyume cha sheria, akiongeza kuwa anatarajia nchi husika kuheshimu sheria za Ujerumani.

Majimbo matatu ya Ujerumani -- Saxony-Anhalt, Berlin na Mecklenburg-Western Pomerania -- yamepangwa kufanya uchaguzi wa majimbo mwezi Septemba. Kura za maoni za hivi karibuni zinaonyesha chama hicho cha AfD kinaongoza katika Saxony-Anhalt na Mecklenburg-Western Pomerania.

Merz pia amesema kwamba kama kuna chama cha mrengo-mkali wa kulia kitakachoingia katika serikali ya Ujerumani, itakuwa na "maana tofauti kabisa" kwa sababu ya kufikiria historia ya Ujerumani, lakini kama hali hii itatokea katika nchi nyingine ya Umoja wa Ulaya, hali ya mambo itakuwa tofauti nayo.

"Nitafanya kila niwezalo kuzuia hali hii isitokee nchini Ujerumani," amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha