Kazi ya kurejesha hali ya kawaida yaendelea baada ya kimbunga kuukumba Mji wa Huanggang, Hubei, China (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 14, 2026
Kazi ya kurejesha hali ya kawaida yaendelea baada ya kimbunga kuukumba Mji wa Huanggang, Hubei, China
Picha hii ya kuunganisha ikionyesha mazingira ya maktaba ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Huanggang katika Mkoa wa Hubei, katikati mwa China, Julai 8, 2026 (juu) na mandhari ya maktaba hiyo Julai 13, 2026 (chini).(Xinhua/Wu Zhizun)

Kati ya saa 1 jioni na saa 5 usiku Julai 6, dhoruba za radi na upepo mkali vilitokea katika miji ya Huangshi, Huanggang, Ezhou, na Xianning, ambapo tarafa mbili zilikumbwa na dhoruba za upepo mkali zilizofikia nguvu ya daraja la 13 katika Mkoa wa Hubei katikati mwa China. Serikali ya huko ilisema, vimbunga vikali vilitokea katika baadhi ya maeneo.

Mkoa wa Hubei umeanzisha kazi kwa pande zote za uokoaji na utoaji misaada ili kulinda maisha na mali za watu. Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya Kitaifa ya China imetenga yuan milioni 50 (dola za Marekani karibu milioni 7.34) kutoka bajeti kuu kwa kusaidia kazi za dharura za kurejesha hali ya kawaida ya miundombinu, ikiwa ni pamoja na barabara, majengo ya shule na majengo ya huduma za umma, na kusaidia maeneo yaliyoathiriwa kurejesha uzalishaji wa kawaida na maisha ya kila siku mapema iwezekanavyo.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha