Lugha Nyingine
Jukwaa la Davos la Majira ya Joto 2026 lafunguliwa katika Mji wa Dalian Kusini-Mashariki mwa China (5)
![]() |
| Washiriki wakizungumza kwenye Mkutano wa 17 wa Mwaka wa Mabingwa Wapya, huko Dalian, Mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China, Juni 23, 2026. (Xinhua/Han He) |
BEIJING - Jukwaa la Davos la Majira ya Joto 2026 ambalo pia linajulikana kwa jina rasmi la Mkutano wa Mwaka wa Mabingwa Wapya wa Jukwaa la Uchumi wa Dunia (WEF) limefunguliwa jana Jumanne mjini Dalian, Mkoa wa Liaoning, kaskazini-mashariki mwa China na limepangwa kufanyika kuanzia Jumanne hadi Alhamisi wiki hii.
Jukwaa hilo linatazamiwa kukutana kwa washiriki zaidi ya 1,700 kutoka nchi na maeneo zaidi ya 90 ili kujadili namna dunia nzima inavyokabiliana na changamoto, na wakati huohuo kuleta fursa mpya za kupata ongezeko jipya la uchumi.
Mada kuu ya mkutano wa mwaka huu ni "Uvumbuzi wa Kiwango," na kuhusisha mijadala juu ya kipindi kijacho cha maendeleo ya uchumi wa China na jinsi ya kubadili maendeleo ya kiteknolojia kuwa ufanisi na manufaa halisi ya kiuchumi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




